Direkt zum Inhalt

Chama Cha Tanzania Network

Tanzania Network ni Shirika lisilo la Kiserikali la Ujerumani lililoanzishwa kama chama mwaka wa 2000; Wanachama ni Watanzania na Wajerumani, vikundi na mashirikia katika siasa, jamii na makanisa, yenye uhusiano wa muda mrefu na wa karibu na Tanzania.Chama cha Tanzania Network e.V. kinajitambua kama shirikisho kuu la Ujerumani linalowaunganisha wadau wanaohusika na masuala ya Tanzania katika nyanja za kijamii, uchumi, siasa, taaluma na watanzania wanaoishi ughaibuni.

Lengo letu ni kuunganisha vikundi vya ushirikiano, wanaojitolea kikazi, wanaopenda Tanzania kwa kubadilishana mawazo kuhusu ushirikiano wa maendeleo endelevu, ubaguzi wa rangi, Mitazamo baada ya Ukoloni na sera za maendeleo. Tunatoa jukwaa la kubadilishana uzoefu na taarifa, kufanya kazi ya ushawishi na utetezi na kukutanisha watu.

Kupitia kazi yetu ya elimu, tunalenga kutoa mitazamo mbalimbali na ya kina, kuhusu mada zianaojadiliwa Tanzania na ambazo zinatuhusu pia hapa Ujerumani. Kwa kazi yetu ya utetezi wa maslahi, tunasisitiza Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGS (Sustanibal Development Goals), kupinga ubaguzi wa rangi, fikra baada ya ukoloni na haki za wanadamu.

Ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania

Jamhuri ya Ujerumani inakadiriwa kua na taasisi kati ya 800 – 1000 zilizo na uhusiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali kama viele: Miji, shule, sharika za makanisa, misheni, makampuni, vyama, vyuo vikuu na taasisi mablimbali. Hii inaonesha kuna mahusiano mengi tofauti yanayoamínika kua na uwezo mkubwa.Wengi wao wanajishughulisha na mada za ulimwengu mzima, sera za maendeleo na ushirikiano endelevu, soko la haki (fair trade), Elimu ya kimataifa, maendeleo endelevu, utamaduni, haki za binadamu, usawa wa kijinsia na mada nyinginezo katika kazi yao ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania.

Kazi zetu

SEMINA (kijerumani/kiingereza): Tuanaandaa semina mbili kwa mwaka kuhusu mada zetu kuu kama vile: uswa wa jinsi, maendeleo endelevu, haki za binadamu n.k. Katika warsha, mihadhara na majadiliano jukwaani, utapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wataalamu na washiriki wengine. Pia tunatoa muda wa kutosha wa kustarehe na kuzungumza pamoja.

HABARI (kijerumani/kiingereza): Ofisi ya mhariri wa jarida la Habari huchapisha hili jarida lenye kurasa 70 hadi 85 mara nne kwa mwaka likiwa na makala zilizoandikwa na waandishi wa Kitanzania na Wakijerumani kuhusu mada kuu ya toleo hilo. Mbali na kutoa mitazamo mingi ya hali ya Tanzania, jarida hili pia huangalia mambo yanayohusu Ujerumani.

NETTALK (kiingereza, kiswahili): Zaidi ya hapo Tanzania Network inaandaa kipindi cha mtandaoni kiitwacho Net Talk, ambapo wataalamu wakitanzania wanajadili kwa kina mada ya utata iliojitokeza. Wasikilizaji wanakaribishwa kusikiliza na kuuliza maswali. Video zinaonekana kwa njia ya YouTube.

MITANDAO YA KIJAMII (kijerumani): Katika mitandao yetu ya kijamii tunatoa taarifa kuhusu matukio ya sasa nchini Tanzania. Tunafanya kazi ya elimu kwa umma, kwa mfano kwa kuonyesha video za tafiti za maoni kuhusu mada zetu au rekodi za matoleo yetu ya kielimu. Hapa utapata pia misemo ya Kanga na maana zake. Tembelea Instagram yetu, tufuate YouTube, au jiunge na Whatsapp, Facebook na Spotify.

Kazi yetu inagharamiwa na ada ya wanachamu, michango na misaada kutoka kwa (Engagement Global, Brot für die Welt na Miserior).

Sisi ni

Kazi zetu za kuelemisha na utetezi wa maslahi mbalimbali ya chama cha Tanzania Network hufanywa na watu wanaojitolea pamoja na walioajiriwa rasmi. Katika ofisi ya uratibu ilioko Berlin,kuna watumishi watatu wa kudumu wanashughulikia masuala ya uratibu na fedha. Wanaojitolea katika Bodi ya Chama, wanaamua kuhusu mada kuu za kisera za maendeleo kwa kila mwaka. Pia wanaandaa semina na midahalo ya Nettalks zetu pamoja na wengine walio na moyo wa kujitolea wakishirikiana na ofisi ya uratibu. Timu ya uhariri wa jarida la HABARI iliyo pia na waandishi wa kujitolea huandaa toleo la jarida la Habari mara nne kwa mwaka.